WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumatatu, 5 Juni 2017

 05:32      No comments


Na Jonas Kamaleki- MAELEZO.

Viongozi wa Dini wanajiandaa kumpa tuzo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi kwa utendaji mzuri uliojaa ubunifu na uwajibikaji.

Hayo yameelezwa katika mahojiano maalum jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadili na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Dini zote Tanzania, Askofu William Mwamalanga.

Askofu Mwamalanga amesema kuwa Waziri Lukuvi amekuwa kiongozi imara katika kufuatilia masuala yanayohusu ardhi ikiwemo utatuzi wa migogoro ambayo imedumu kwa muda mrefu.

“Lukuvi ameing’arisha Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuendana na kasi ya Rais John Pombe Magufuli, hakika amevaa viatu vya Magufuli, hivyo tumeamua kumpa tuzo maalum kwa ajili utendaji wake”, alisema Askofu Mwamalanga.

Ameeleza kuwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imefanya jambo zuri kwa kutoa elimu ya ardhi kiasi kwamba karibu kila mtu amefahamu matumizi ya ardhi na umuhimu wake.

Askofu Mwamalanga amesema kuwa ardhi imefanywa kuwa lulu na kufanya sura mpya ya ardhi kuonekana ambapo takriban asilimia 85 ya Watanzania wameiona kuwa ni mali.

Mhe. Lukuvi amewapa nafasi ya kwanza wananchi kuliko Sheria jambo ambalo limewafanya Watanzania kujisikia kuwa wanathaminiwa na Serikali yao, aliongeza Askofu Mwamalanga.

Kiongozi huyo wa Dini amesema kuwa Mhe. Lukuvi ni mfano wa kuigwa na mawaziri na viongozi wenzake kwa uchapakazi wake. Amesema kuwa ni Waziri ambaye anawashirikisha watendaji waliochini yake katika maamuzi mbali mbali, hivyo anastahili kupewa tuzo.

“Tumepanga kumpa tuzo Waziri Lukuvi kwa kuzingatia yafuatayo: Kuiweka ardhi mikononi mwa watanzania, kuonyesha kuwa ardhi ni chanzo kikuu cha uchumi wa watu na utatuzi wa migogoro ya ardhi hasa iliyodumu kwa muda mrefu”, alisema Askofu Mwamalanga. 

Migogoro hiyo ni kama vile mgogoro wa kijiji cha Mabwegere, Mkoani Morogoro, mgogoro wa Chasimba, jijini Dar es Salaam na migogoro mingine mingi katika mikoa ya Arusha, Mbeya, Kigoma, Tanga na Mwanza.

Askofu Mwamalanga amesema Kamati yake imewasiliana na Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi ili watoe mapendekezo ya tuzo ambayo anastahili kupewa Mhe. Lukuvi kwa utendaji kazi wake mzuri. 

Amezitaja baadhi ya Taasisi hizo kuwa ni Vyuo Vikuu vya Umma na Binafsi, Marais wastaafu na mawaziri wakuu wastaafu, Vyama vyote vya siasa ambavyo kwa ujumla wake vimeonyesha kutambua mchango wa waziri Lukuvi.

Baada ya kupokea mapendekezo na kuyafanyia kazi ndipo itatangazwa siku ya kutoa tuzo hiyo kwa Mhe. Lukuvi, alisema Askofu Mwamalanga.

Tangu Waziri Lukuvi aiongoze Wizara ya ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi mwisho mwa uongozi wa awamu ya Nne hadi sasa, 

mabadiliko yenye tija katika wizara hiyo yameonekana. Migogoro mingi ya ardhi imetatuliwa, utoaji wa hati za viwanja umerahisishwa na huduma kwa wateja imeboreshwa.

DC SOPHIA MJEMA APONGEZA JITIHADA ZINAZOFANYWA NA CHUO CHA ST.MARK KATIKA KUELIMISHA JAMII

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akizungumza na wanajumuiya ya Chuo cha St. Mark kilichopo Buguruni Malapa alipofanya ziara ya kikazi chuoni hapo.Kulia kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo Dr. Peter Kopweh na kushoto ni Mshauri wa majeshi ya akiba Chripin Makota.
Wanajumuiya ya Chuo cha St. Mark kilichopo Buguruni Malapa wakimsikilia Mh.Sophia Mjema alipofanya ziara ya kikazi chuoni hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akianza ziara kuzuru maeneo mbalimbali yaliyopo katika mazingira ya chuo cha St.Mark akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama pamoja na timu ya wataalamu wa wilaya ya Ilala.



Na Dickson Mulashani

Mkuu wa wilaya Ilala Mh. Sophia Mjema amekipongeza Chuo cha St Mark (Chuo Kikuu Kishiriki Cha St Joseph) kwa jitihada za kutoa elimu bora kwa manufaa ya wilaya na Taifa kwa ujumla alipofanya ziara ya kikazi chuoni hapo mwishoni mwa juma.

Akiwasili chuoni hapo Mh. Sophia Mjema alikuwa ameambatana na ujumbe wa timu ya wataalamu katika ngazi mbalimbali a wilaya ya Ilala akiwemo Mratibu Mwadamizi wa Polisi, Mshauri wa Majeshi ya akiba, Mratibu wa Magereza, Mhandisi , Afisa uhamiaji, Afisa Elimu Taaluma, Afisa mipango miji, Afisa ustawi wa jamii, Afisa wa Benki ya NMB, Afisa Tarafa, Diwani pamoja na Mwenyekiti wa mtaa.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha St. Mark Dr.Peter Kopweh akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa wilaya alipokuwa akizuru maeneo mbalimbali katika chuo hicho.

Akimkaribisha mgeni huyo, kaimu Mkuu wa Chuo Dr.Peter Kopweh alianza kwa kuelezea historia fupi ya chuo hicho kilichopo eneo la Buguruni Malapa jirani na shule ya msingi viziwi, kuwa ni sehemu ya Chuo Kikuu cha St. John’s chenye makao yake makuu mjini Dodoma ambacho kinatoa kozi katika ngazi astashada na shahada za sanaa katika elimu, utawala wa biashara, rasilimali watu, elimu na biashara pamoja na theolojia mathalani shahada ya uzamili katika elimu hili kwa ushirikiano na kampasi mama ya Dodoma.

Sambamba na ukaribisho huo Dr. Kopweh hakusita kuelezea Changamoto zinazokikabili chuo hicho zikiwemo za miundombinu ya barabara, usalama wa mali pamoja na wadau wake kadhalika suala la mipaka ambayo inaonekana kuingiliwa na wakazi wanaozunguka chuo hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mipango Miji Ilala Bw. Benjamin Chagula wakati akiangalia namna ya kutatua Changamoto ya mipaka ya chuo hicho inaingiliwa na wananchi wanaoishi eneo jirani.

Nae katika hotuba yake Mh.Mjema ambaye alipata fursa ya kuzungukia maeneo kadhaa chuoni hapo alieleza lengo kuu la kufika chuoni hapo kadhalika kupongeza uongozi wa chuo hicho kwa jitihada zinazofanyika.

“Nimeamua kutoka na kuja kuwaona kwani nauthamini sana uwepo wenu katika wilaya yangu (Ilala) kwani hii ni fursa muhimu ya serikali kuwatumia wasomi hata waliopo vyuoni kutatua Changamoto katika maeneo waliyopo, mimi nakazia hapa wilayani na naamini ujio huu utakuwa wenye tija sana kwetu sisi pamoja nanyi kama taasisi katika kushirikiana” alisema Mh. Sophia Mjema.

Kadhalika akizungumza na wanafunzi pamoja na wafanyakazi wa chuo hicho, Mh.Mjema alitangza kufungua milango ya fursa kwa wasomi hao kufika ofisini kwake na kuleta mawazo pamoja na nguvu zao ili kusukuma gurudumu la maendeleo mbele huku akikazia suala la uzalendo pamoja na wito wa Mh Rais Magufuli kuhusu kufanya kazi.

Vilevile Mh. Mjema alikazia suala la kuimarisha misingi ya elimu ya juu kwa kuwekeza kwenye uboreshaji wa teknolojia kwani dunia ya sasa mitandao umekuwa nyenzo muhimu ya kupata taarifa za kitaaluma.

“Mkakati wa kusambaza huduma ya intaneti (WIFI) katika vyuo vikuu hapa Ilala unaendelea kwa kasi na umesimama kwa muda kutokana na hali ya mvua lakini baada ya hali hii kila kitu kitakuwa kama ilivyoahidiwa,lazima msome kisasa” alihitimisha.

Nae Rais wa chuo kwa niaba ya wanafunzi wote alifikisha Changamoto zinazowakabili ikiwemo suala la mikopo pamoja na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara kwani limekuwa likidhohofisha maendeleo ya taaluma alitoa shukrani kwa mkuu wa wilaya na kuahidi ushirikiano na ofisi ya wilaya pamoja na kujitoa kutumia taaluma zao ndani ya jamii kwa ujumla.

Akihitimisha zoezi hili pamoja na kumshukuru Mh.Mjema kwa kufika chuoni hapo, Kaimu Mkuu wa Chuo alitoa wito kwa watanzania kujiunga na Chuo hicho hasa wakati huu ambapo milango ipo wazi kwa wanafunzi kudahiliwa vyuoni moja kwa moja huku akiwaondoa hofu wale wanaobanwa na kazi kuwa watapata fursa ya kusoma masomo ya jioni.

SHINDANO LA SPRITE BBALL KINGS LAINGIA HATUA YA 16 BORA

Na Torinto Hot Blog.


Shindano la Sprite Bball Kings 2017  limeingia katika hatua ya 16 baada ya timu 52 kukipiga wikiendi hii ikiwa ni ufunguzi wa michuano hiyo

Michezo hiyi 26 iliyochezwa katika viunga vya viwanja vya Jakaya M Kikwete Park (JKM Park) na kuzikutanisha timu hizo 52 katika mechi 26 za mtoano na 16 kufanikiwa kuingia hatua inayofuata.

Akitoa tathmini ya michuano hiyo Mratibu wa Sprite Bball Kings Basilisa Biseko amesema kuwa hatua ya mtoano imefanyika wikiendi hii na timu 16 kufanikiwa kuingua hatua inayofuata ila katika mechi hizo kuna baadhi walipewa ushindi wa mezani.

Basilisa amesema kuwa kuna baadhi ya timu hazikufanikiwa kufika siku hiyo na  ratiba ilikuwa tayari imeshapangwa katika droo iliyokuwa imemipangwa na kupelekea timu iliyokuwa imefika uwanjani kupatiwa ushindi wa mezani.


"Katika michezo 26 iliyochezwa siku ya Jumamosi katika viwanja vya JMK Park timu 16 zimefanikiwa kuingia hatua ya 16 bora ila kuna timu zingine zimeingia kwenye hatua hiyo bila kucheza na timu pinzani kutokana na mpinzani wake kutokufika na kupelekea kupewa alama zitakazomruhusu kuingia hatua inayofuata,"amesema Basilisa.

Amesema kuwa, kwa timu zilizopata alama nyingi ndizo zilizofanikiwa kuingia katika hatua ya 16 bora na mashindano hayo yataendelea tena ili kumpata mshindi wa Sprite Bball Kitaa kwa mwaka 2017.
 Timu zilizofuzu kuingia hatua ya 16 bora katika shindano la Sprite Baball Kings 2017 ni DMI, Dream Chaser, UDSM, Oysterbay, Ukonga Warriors, The Fighter, Ardhi na Bongo Hits.

Timu zingine ni Chanika Legends, Montfort, Heroes S/B, Kigamboni Heroes, TMT, Mchenga, Kurasini na Landforce.

Mashindano ya Bball Kings mwaka huu yanadhaminiwa na Sprite wakishirikiana na kituo cha East Africa Redio na TV  na yalizinduliwa mapema mwezi wa tano na kuanza usaili kwa wilaya za Teemek, Kindondoni na Ilala na kupata timu 4.52 zilizojitokeza kushiriki shindano hilo.
Timu ya mpira wa kikapu ya UDSM wakiw akatika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mtangange wao.
 Timu ya mpira wa kikapu ya UDSM (jezi ya njano) wakipambana na katika hatua ya mtoano ya shindano la Sprire Bball Kings iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii katika viwanja vya  Jakaya M Kikwete Park (JKM Park).
 Mashabiki na timu zingine zilizoshiriki katika  hatua ya mtoano ya shindano la Sprire Bball Kings iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii katika viwanja vya  Jakaya M Kikwete Park (JKM Park) wakiwa jukwaani wakifuatilia baadhi ya michezo mingine.
Timu za mpira wa kikapu wakiwa wanachuana katiika shindano la Sprire Bball Kings iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii katika viwanja vya  Jakaya M Kikwete Park (JKM Park).

Kamishna wa Ufundi na Uendeshaji Mashindano wa chama Shirikisho la Mpira wa Kikapu (TBF) na Mratibu  wa Sprite BBall Kings Manase Zablon  (kushoto) akiwa pamoja na mtangazaji wa East African Drive David Rweganyira wakichambua baadhi mechi zilizokuwa zikiendelea.

KAMPUNI YA ACACIA YACHANGIA KATIKA HARAKATI ZA GGM KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA MAPAMBANO YA VITA DHIDI YA UKIMWI.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Tulia Ackson akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika lango la kupandia mlima Kilimanjaro,lango la Machame kwa ajili ya kutoa Baraka kwa washiriki wa changamoto ya kupanda mlima kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi zoezi linaloratibiwa na Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM).
Mgeni rasmi katika shughuli ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za mapambano Vita ya Ukiwmwi ,Dkt Tulia Ackson akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mshikizi ,Mrisho Gambo (kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ukimwi na Dawa za kulevya ,Dkt Faustine Ndugulile wakiimba wakipiga makofi.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Tulia Ackson kizungumza wakati wa kutoa baraka kwa wanaharakati 89 wakiwemo wafanyakazi wa Kampuni ya Acacia wanaoshiriki zoezi panda mlima kwa lengo lakuchangisha fedha kwa ajili ya mapambano ,vita dhidi ya Ukimwi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM) Terry Melpeter akizungumza katika shughuli hiyo iliyofanyika katika lango la Machame.
Baadhi ya viongozi wa wilaya za Hai na Moshi mjini wakifuatalia  shughuli hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mshikizi Mrisho Gambo akizungumza wakati wa shuguli hiyo ambayo hufanyika kila mwaka.
Msanii Mrisho Mpoto ambaye ni Balozi wa TACAIDS akitoa burudani kwa washiriki wa changamoto hiyo.
Kampuni ya Acacia ,wamiliki wa Migodi ya Buzwagi,Bulyanhulu na North Mara ni miongoni mwa kampuni ambazo zimekua zikitoa michango yao kusaidia kampunu ya GGM katika mapambano ya vita dhidi ya Ukimwi ambapo wafanyakazi wake pia ni miongoni mwa wanaharakati waliopanda Mlima Kilimanjaro.
Naibu Spika Dkt Ackson akisalimana na Meneja wa Benki ya NMB,tawi la Moshi ,Emanuel Kishosha kabla ya kuanza kwa zoezi la kupanda mlima Kilimanjaro.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Acacia wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Spika ,Dkt Ackson kabla ya kuanza kwa zoezi la kupanda mlima.
Zoezi la kuapnda Mlima likianza rasi huku likiongozwa na Naibu Spika ,Dkt Tulia Ackson ,Mrisho Mpoto akiongoza kwa nyimbo za kuhamasisha.
Zoezi la kupanda lilianza huku mvua ikinyesha,

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

Vijana waungana kuendeleza elimu ya afya ya uzazi baina yao



Wanachama wa Taasisi za YAM – UMATI Johnbest Mwahaja (kushoto) na ZAFAYCO Amnah Ibuni (kulia) wakisaini makubaliano ya kuwa taasisi moja ya Tanzania Youth and Adolescent Reproductive Health Coalition (TAYAHR) ambao itakuwa na jukumu kutoa elimu ya uzazi wa mpango na afya ya uzazi kwa vijana wa Tanzania.

Wanachama wa Taasisi za AFRIYAN Fatma Said Ahmed (kushoto) na Hope Centre for Children, Girls and Women in Tanzania Penina Mgonela (kulia) wakisaini makubaliano ya kuwa taasisi moja ya Tanzania Youth and Adolescent Reproductive Health Coalition (TAYAHR) ambao itakuwa na jukumu kutoa elimu ya uzazi wa mpango na afya ya uzazi kwa vijana wa Tanzania.

Mwanachama wa Taasisi za AFRIYAN Fatma Said Ahmed (kushoto) akibadilishana mkataba na Mwenyikiti wa Taasisi ya Tanzania Youth and Adolescent Reproductive Health Coalition (TAYAHR) chairperson William Otuck baada ya kutia saini ya makubaliano ya kufanya kazi chini ya taasisi hiyo yenye lengo ya kutoa elimu ya uzazi wa mpango na afya ya uzazi kwa vijana wa Tanzania.

Jumla ya taasisi kumi za vijana zimeungana ili kuzidisha nguvu ya kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wenzao nchini Tanzania na zaidi ikilenga matumizi ya mpango wa uzazi. Vijana hao wamejizatiti kuhahakisha kuwa kuna uwekezaji wa kutosha kwenye elimu juu ya uzazi wa mpango na pia vijana kuhusisha kwenye maamuzi yanayohusu vijana na afya ya uzazi.

Taasisi hizo zimetiliana saini makubaliano na kuwa taasisi moja ikayoitwa Tanzania Adolescent and Youth Reproductive Health (TAYAHR) jana jijini Dar es Salaam ambapo taasisi hiyo itajikita zaidi kwenye kutoa elimu, kuhusisha vijana na kuhakikisha huduma inafika kwenye maeneo sahihi kwa muda sahihi.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutia saini makubaliano hayo, Mwenyekiti wa TAYAHR William Otuck alisema Tanzania ina changamoto kuona ya kwamba asilimia 27 ya vijana wenye miaka 15-19 wana mtoto au ni wajawazito huku utumiaji wa uzazi wa mpango na hasa vidonge vya uzazi kati yao ikiwa ni chini sana – yaani asilimia 13 peke yake huku pia wakiwa hawana elimu yeyote kuhusu afya ya uzazi na hivyo kukosa uamuzi sahihi kwenye masuala ya kujamiiana.

‘Robo ya wasichana wenye umri kati ya 15 na 19 Tanzania wana watoto au ni wajawazito na hali ni mbaya kwenye mkoa wa Katavi yenye asilimia 45 na Tabora asilimia 42 kwa wasichana wenye umri huo. Hii inamaanisha kuna idadi kubwa ya wasichana ambao wanakatisha masomo na kuingia kwenye hali ya kuwa mzazi wangali wana umri mdogo na hii kwa kiasi kikubwa uchangia kuongeza hali ya umasiki kwenye jamii’, alisema Otuck huku akiongeza kuwa idadi kubwa ya wasichana wadogo wakipata mimba pia kunachangia kuongezeka vifo vitokanavyo na uzazi.

Akizungumzia kuhusu elimu na hali ya kupata mimba za utotoni, Otuck alisema tafiti zinaonyesha kuwa ni asilimia 10 wa wasichana ambao wana elimu mpaka ya sekondari ambao hupata mimba wakiwa na umri mdogo kulinganisha na wale wana elimu ya msingi ambao ni asilimia 34 na wale ambao hawana elimu kabisa ni asilimia 52.

Taasisi hiyo chini ya uongozi wa vijana pia imelenga kuhamasisha wenye kutoa maamuzi (policy makers) kuwekeza kwenye kupanua wingo la matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango ili kufikia walengwa ambao bado hawajafikia, ambapo kwa sasa inaonyesha asilimia 23 ya wanawake vijana wanatamani kutumia uzazi wa mpango lakini bado huduma hiyo
haiwajafikia na pia kuongeza matumizi ya uzazi wa mpango kwa vijana angalau kufikia asilimia 80 ifikapo 2010 na pia kuendeleza elimu ya afya ya uzazi kwa vijana.

Taasisi hizi kabla ya kufikia makubaliano yao zilianza mazungumzo mwezi Oktoba na Novemba mwaka jana chini ya FP2020 Secretariat, mradi wa Advance Family Planning (AFP) Tanzania pamoja na taasisi ya Torchlight Collectives. TAYAHR inaundwa na taasisi za Hope Centre for Children, Girls and Women in Tanzania, YAM-UMATI, AfriYAN, TYVA, SAYI, Restless Development, Zanzibar Youth Forum (ZAFAYCO), IYAFP/Young and Alive Initiative (YAAI), SHDEPHA+ na YUNA.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *